Trump ataka kumbana zaidi Rais Maduro

Rais Nicolas Maduro, anayelalamikiwa na Marekani

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Rais Nicolas Maduro, anayelalamikiwa na Marekani

Rais wa Marekani Donald Trump amesisitizia wito wa kurejesha katika hali ya kawaida uhuru wa kisiasa na demokrasia nchini Venezuela.

Akizungumza na viongozi wa Amerika ya kusini mjini New York, Rais Trump amesema atachukua hatua zaidi, dhidi ya kile alichokiita utawala wa kidikteta wa Rais Nocolas Maduro.

Amesema watu wa Venezuela wamekuwa wakikosa chakula na nchi yao kizidi kuharibika, licha ya awali kuwa ni nchi tajiri.

Mwezi uliopita serikali ya Marekani iliiwekea Venezuela vikwazo vipya vya kifedha.

Aidha ilimuwekea pia vikwazo Rais Maduro na baadhi ya wasaidizi wake wa karibu, kwa kile ilichokiita kuwa ni diktekta.