Kwa Picha: Mitindo ya mavazi katika tuzo za Emmy

Tuliwaona nyota waliotia fora kwa mavazi ya kupendeza zaidi katika tuzo za Emmy TVmwaka huu mjini Los Angeles.

Reese Witherspoon

Chanzo cha picha, Getty Images

Reese Witherspoon, mmoja wa wachezaji filamu nyota katika Big Little Lies, alivalia tuxedo, ya Stella McCartney. Big Little Lies ilikuwa moja ya washindi wakubwa katika hafla hiyo iliyofanyika usiku , ikiibuka na tuzo tano za ushindi . msanii mwenza wa Reese , Nicole Kidman, alimshinda kwa kuchukua tuzo la mchezaji filamu bora zaidi

Chanzo cha picha, Getty Images

Zoe Kravitz, pia ni wa Big Little Lies, aling'ara kwa vazi la Dior haute. Zoe ambaye ni binti yake Lenny Kravitz na Lisa Bonet alicheza kama Bonnie, ambaye alikuwa mke wa pili wa mwanamume ambaye awali alimuoa mtu aliyeitwa Witherspoon

Chanzo cha picha, Getty Images

Donald Glover alitamba kwenye zulia jekundu katika suti hii ya zambarau ukipenda -aubergine tux. Nyota huyu wa Atlanta alinyakua tuzo mbili, moja akiipata kwa kuwa muongozaji bora wa kipindi cha vichekesho. Ni mmarekani wa kwanza mweusi kuwahi kunyakuwa la aina hiyo

Chanzo cha picha, Getty Images

RuPaul (pichani akiwa na mtangazaji wa TV Michelle Visage) pia alitinga suti nyeusi ya tuxido iliyotengenezwa na harlequin. RuPaul alikuwa akiwania tuzo la mtu mwenye kipindi kizuri zaidi cha Televisheni cha maisha halisi lakini hakubahatika kupata

Chanzo cha picha, Getty Images

Lena Waithe aliweka historia kwa kuwa mMarekani wa kwanza mweusi mwanamke kupata ushindi kwa uandishi wa wa vichekesho . Alipata tuzo kwa kushirikiana katika uandishi wa kipindi cha Master of None pamoja na Aziz Ansari, mbunifu mwenza wa kipindi cha Netflix serie na nyota wa kipindi hicho. KIpindi hicho kiliandaliwa kwa kuzingatia maisha halisi ya Waithe

Waithe, ambaye pia alishiriki katika onyesho hilo , alisema katika kauli yake ya kukubali tuzo lake : "Kwa ajili ya familia ya LGBTQIA ,ninamuona kila mmoja wenu. Mambo yanayotufanya tuwe tofauti , ndio nguvu yetu kubwa ."

Chanzo cha picha, Getty Images

Nyota Noah Schapps aliwashangaza wengi kwa vazi hili la suti la kitambaa cha velvet. Noah mwenye umri wa miaka 12-anacheza kama Will Byers katika show ya Netflix , ambayo iliambulia patupu kwa kukosa tuzo hata moja.

Chanzo cha picha, Getty Images

Ungependa mshono huu? Huyu ni Evan Rachel Wood ambaye aliamua kuwa na muonekano huu kwenye hafla ya Tuzo za Emmy mwaka huu . Nyota huyu wa Westworld aliteuliwa kwa kuwa mchezaji filamu anayeongoza katika kipindi cha tamthilia cha TV lakini hakufanikiwa kupata tuzo hilo lililoendea kipindi cha The Handmaid cha Elisabeth Moss.

Chanzo cha picha, Getty Images

Nicole Kidman aling'ara katika vazi hili la Calvin Klein linalotoa picha ya muonekano wa tangu jadi wa urembo wa Hollywood . Aliweza hata kuonyesha viatu vyake vya wazi ambavyo havikufanana na gauni lake - nani alisema alikwambia rangi nyekundi na waridi haviendani?

Katika Kundi A-la nyota wa filamu , ni mchezaji filamu ambaye aliweza kufanikiwa kuhamishiwa katika screen ndogo, alitajwa kama mchezaji filamu bora zaidi wa kike katika kuipindi kifupi cha tamthilia ya TV kwa nafasi yake katika kipindi cha Big Little Lies.

Chanzo cha picha, EPA

Claire Foy ambaye alionekana hakuweka juhudi kubwa ya kutafuta vazi la siku aliwapungia mkono waliofika kushiriki hafla ya Emmy akiwa ametinga vazi la jumpsuit lilitengenezwa na Oscar de la Renta. John Lithgow, ambaye ni nyota mwenza katika The Crown, alipokea tuzo la mchezaji filamu msaidizi aliye bora zaidi.

.