Baadhi ya Apps za iPhones na ipads za Apple zitasita kufanya kazi

Apple inajaribu kwa juhudi zote kuwalazimisha wateja wake kuendana na kasi yake

Chanzo cha picha, PENGUIN

Maelezo ya picha,

Apple inajaribu kwa juhudi zote kuwalazimisha wateja wake kuendana na kasi yake na kuwafanya watu wasonge mbele na teknolojia yake

. Wamiliki wa simu za iPhones na iPads waliotengeneza toleo la hivi karibuni la mfumo wa simu ya mkononi ya Apple watabaini kuwa baadhi ya apps za zamani zitasita kufanya kazi.

Hatua hiyo itaathiri kwa ujumla apps ambazo zimekuwa hazijafanyiwa marekebisho mapya kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita.

Ingawa nyingi zitaacha kutumiwa na wabunifu wake, wamiliki wake bado wataendelea kutumia baadhi yake mara kwa mara.

Haya ni matokeo ya kudhibitiwa kwa iOS 11 kuendesha apps zilizoandikwa katika kile kinachofahamika kama 64-bit code.

Namba hii inaonyesha ni kwa kiwango gani cha data kinachoweza kutengezwna ambacho kinaweza kutunzwa na simu - kadri namba inavyokuwa kubwa zaidi ndivyo kompyuta inavyokuwa na uwezo wa kufanya kazi.

Kushuka kwa kiwango cha data 32-katika software huifanya Apple kuchuja mifumo yake ya utendaji na huisaidia kufanya kazi haraka zaidi kwasababu haitahitaji tena kujaza maktaba za software kwa ajili ya kuziwezesha apps za zamani kufanya kazi.

Baadhi ya Apps zifuatazo zinaweza kusababisha i Pad yako kuzorota na hazitafanya kazi na iOS 11, ikiwa hazijaboreshwa:

Maelezo ya picha,

Apple imewezesha utambuzi wa apps ambazo zitasita kufanya kazi kabla ya kuwekwa kwa iOS 11

Awali Apple ilielezea kwamba ni rahisi kiasi kwa watengenezaji wa app kutengeneza upya bidhaa zake, na hifadhi yake ya App imekataa kutengeneza bidha asilia zenye upya ambazo hazina usaidizi wa 64-bit tangu Juni 2015.

Hata hivyo, hatua hiyo inalinda mifumo ya utendaji wake katika kusaidia kudumisha ubora wa software kwa kipindi kirefu.

"miaka miwili ni kipindi kifupi kwa kitu kushindwa kufanya kazi, hata katika ulimwengu wa teknolojia ambako mambo yanabadilika haraka ,"alisema Profesa Alan Woodward, kutoka Chuo kikuu cha Surrey idara ya masomo ya Kompyuta.

" Kile ambacho wauzaji wa rejareja wamefanya kwa sasa na - Microsoft ni mfano mzuri wa hili - kutunza mambo mengi kwa urahisi iwezekanavyoili mradi inawezekana kufanya hivyo.

"isingelichukua kazi kubwa kwa iOS 11 kuwa na usaidizi endelezi wa 32-bit, kwa hivyo si rahisi kutokubali kwamba Apple inajaribu kwa juhudi zote kuwalazimisha wateja wake kuendana na kasi yake na kuwafanya watu wasonge mbele na teknolojia yake''. Amesema Profesa Alan Woodward