Msanii Msafiri Zawose achaguliwa kuwania Tuzo za Afrima
Huwezi kusikiliza tena

Msanii Msafiri Zawose amechaguliwa kuwania Tuzo za Muziki za Afrika, Afrima

Msanii Msafiri Zawose amechaguliwa kuwania Tuzo za Muziki za Afrika, zinazofahamika kwa jina la Afrima katika kipengele cha muziki wa Asili na kuwa ndio mwanamuziki wa kwanza kutoka Tanzania kuchaguliwa katika kipengele hicho kinachohusisha muziki unaotumia ala za asili kama vile marimba, zeze na hata filimbi. Tuzo hizi kubwa za Muziki barani Afrika zitatolewa nchini Nigeria mwezi November mwaka huu. Mwandishi wetu Omary Mkambara ametuandalia taarifa ifuatayo.