Mtoto aliyehai agunduliwa kifusini

juhudi za uokoaji zikiendelea Haki miliki ya picha Authority
Image caption juhudi za uokoaji zikiendelea

Waokoaji katika mji wa Mexico city wanajaribu kumfikia msichana mdogo, aliye hai chini ya kifusi cha jengo la shule, lililoporomoka wakati wa Tetemeko la ardhi lililotokea jana.

Wamekuwa wakimpitishia chakula na maji, wakati wakijaribu njia ya kuweza kumtoa salama kutoka katika maangamizi hayo.

Watoto wapatao 21 wamekufa baada ya jengo walilokuwamo kuvunjika, huku wengine wakiwa bado ndani ya kifusi hicho.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wengine tetemeko liliwakuta wakiwa kanisani

Jumla ya watu mia mbili na 25 wamefariki kutokana na tetemeko hilo.

Rais wa Mexico Enrique Pena Nieto amesema kila dakika imekuwa ikihesabika katika kuokoa maisha.

Tetemeko hilo la ardhi ni la pili kuipiga nchi hiyo mwezi huu.