Msichana aliyebakwa na walimu India mahututi baada ya kutoa mimba

Maandamano ya kupinga ubakaji nchini Undia Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Matukio ya kutisha ya ubakaji yamekuwa yakisababisha maandamano nchini India katika miaka ya hivi karibuni

Msichana wa India ambaye alidaiwa kubakwa na walimu wawili wa shule katika kipindi cha wiki tatu yuko katika hali mahututi baada ya kulazimishwa kutoa mimba.

Madaktari wameiambia BBC idhaa ya Hindi kuwa ubongo wake umeharibika.

Polisi imemtioa nguvuni Mkuu wa shule yake na mwalimu wake katika jimbo la kaskazini mwa India la Rajasthan.

Polisi wanasema kuwa alipoteza fahamu baada ya washukiwa skumlazimisha kutoa mimba katika hospitali ya kibinafsi.

Pol;isi pia wanachunguza nafasi ya hospitali katika tukio hilo.

Msichana huyo mwenye umri wa miaka 18 alilazwa hospitalini baada ya kuhisi maumivu makali ya tumbo na wahudumu katika shule yake wakabaini kwamba alikuwa mjamzito.

Mwathiriwa wa ubakaji wa miaka 13 India aiomba mahakama kutoa mimba

Gurmeet Ram akutwa na hatia ya ubakaji

Mvulana aliyebaka India kuhukumiwa

Hali yake ya afya ilianza kuwa mbaya kwa haraka baada ya kuavia mimba, lakini haijafahamika wazi ni nini hasa kilichoifanya hali yake kuwa mbaya,alisema polisi katika wilaya ya Sikar said.

Shule hiyo iliyopo wilaya ya Sikar, imefungwa kwa sasa na mamlaka katika eneo hilo.

Polisi wanaamini kuwa masomo ya ziada yanayotolewa katika saa ambazo si za kawaida yalitumiwa kuwaita wanafunzi ili kuwezesha vitendo kama hivyo vya unyanyasaji kufanyika.

Bado polisi hawajaweza kurekodi taarifa kutoka kwa muathirika.

"Hili ni tatizo baya na hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wahusika ,"alisema afisa wa polisi Kushal Singh.