Msigwa aachiwa baada ya kukamatwa na Polisi Tanzania

Peter Msigwa Haki miliki ya picha Twitter @MsigwaPeter
Image caption Mbunge wa Iringa Peter Msigwa

Polisi mjini Iringa imemuachia mbunge wa Iringa mjini Peter Msigwa kwa sharti la kumtaka arudi polisi Jumatatu.

Taarifa zinasema mbunge huyo ambae pia ni mchungaji wa kanisa alikamatwa pindi alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara katika eneo la Mlandege huko Mkoani Iringa.

Kwa mujibu wa msemaji wa Chadema Tumaini Makene, polisi inadai kumkatama Msigwa kwa tuhuma za uchochezi.

Msingwa anatoka chama cha Chadema ambacho ndio chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania.

Katika siku za hivi karibuni, kumekuwa na kamata kamata ya wabunge nchini Tanzania kutoka upinzani hasa Chadema.

Miongoni mwa waliokumbwa na kamata hiyo hivi karibuni ni mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ambae hivi sasa yuko nchini Kenya kwa ajili ya matibabu baada ya kupigwa risasi na watu ambao mpaka sasa hawajafahamika huko Dodoma, bungeni.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii