Jaji mkuu wa Kenya David Maraga akaribishwa kwa shangwe Dar es Salaam

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Jaji mku wa Kenya David Maraga

Jaji mkuu nchini Kenya David Maraga, ambaye alipata umaarufu kote duniani baada kufanya uamuzi wa kihistoria wa kufuta matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwezi Agosti nchini Kenya, amekaribishwa kwa shangwe kwenye mkutano wa kikanda kwa mujibu wa gazeti ya Citizen nchini Tanzania.

Gazeti hilo linaripoti kuwa Maraga alishangiliwa na washiriki wakati wa mkutano wa majaji ya mahakimu ambao unafanyika mjini Dar es Salam nchini Tanzania.

Bw. Maraga ambaye alisifiwa na wakati huo huo kulaumiwa kutokana na uamuzi wa kufuta matokeo ya kura, amewaambia wale wanaomkosoa kuwa yuko tayari kulipia gharama ya kutetea sheria.

Jaji mkuu nchini Tanzania Prof Ibrahim Juma, alimpongeza Bw. Maraga kwa kutetea uhuru wa mahakama nchini Kenya.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii