Wanawake 100: Wanawake walio orodha ya BBC mwaka 2017

Rais Sirleaf Johnson, ,mwanaanga Peggy Whitson na mcheza soka wa Uingereza Steph Houghton. Haki miliki ya picha iStock
Image caption Rais Sirleaf Johnson, ,mwanaanga Peggy Whitson na mcheza soka wa Uingereza Steph Houghton.

Wanawake hawa ni miongoni mwa wale 100 walioteuliwa na BBC kote duniani kwa mchango wao katika masuala ya ya kulinda na kupigania haki za wanawake .

Image caption Adele Onyango ni mtangazaji wa redio nchini Kenya
  • 1.Adelle Onyango

Adele Onyango ni mtangazaji wa redio nchini Kenya anasema kuwa wanawake wa Afrika kwa jumla wanapaswa kujua kwamba ni sawa kuwa vile walivyo, kuona vili walivyo kama uwezo na kuwa huru dhidi ya hofu na ukimya. Adele anapenda kuwawezesha vijana wa kike kupitia ushauri na kuwafunza

  • 2.Anita Nderitu

Ana umri wa miaka 27, na ni mtangazaji wa runinga na habari katika idhaa ya Capital fm. Anasema ''Wanapokwenda chini tunapanda''-Michelle Obama. Bi Nderitu anapenda kuwashauri vijana.

Image caption Bi Mwaura ni mwanzilishi wa Flone initiative na afisa wa mawasiliano ITDP Afrika nchini Kenya
  • 3.Naomi Mwaura

Bi Mwaura ni mwanzilishi wa Flone initiative na afisa wa mawasiliano ITDP Afrika nchini Kenya. Anasema kuwa wanawake wanahitaji njia nzuri ya kuishi duniani bila ya hofu ya ghasia. Tunafaa kuwa na uwezo wa kuwa mtu yeyote yule.

Akiwa Mwanaharakati Naomi alikuwa mmojawapo ya waandalizi dhidi ya unyanyasaji #MyDressMyChoice ambayo ilibadilisha sheria ya unyanyasaji nchini Kenya.

Image caption Rais wa Liberia Sirleaf Johnson
  • 4.Ellen Sirleaf Johnson

Ana miaka 78 na ni rais wa Liberia. Anasema kuwa ''iwapo ndoto zako hazikugutushi basi ujue sio kubwa''.Ellen ni rais sasa wa Liberia tangu 2006 na rais wa kwanza mwanamke nchini Afrika.

Image caption Talent Jumo mwenye umri wa miaka 36 kutoka Zimbabwe ni mwazilishi na mkurugenzi wa shirika la Katswe Sistahood
  • 5.Talent Jumo

Talent Jumo mwenye umri wa miaka 36 kutoka Zimbabwe ni mwazilishi na mkurugenzi wa shirika la Katswe Sistahood .

Anasema kuwa siko huru wakati kila mwanamke hayupo huru. Hataiwapo matatizo yake ni tofauti na yangu. Mwanaharakti huyo wa Zimbabwe huwasaidia waathiriwa wa ngono ya kulipza kisasi akiwapatia ushauri nasaha pamoja na ule wa kisheria mbali na kupigania haki za wanawake wanaonyanyaswa kingono na kutoa elimu ya uzazi miongoni mwa wanawake wa Zimbabwe.

Image caption Chaima Lasini ni Mwanahabari nchini Morocco
  • 6.Chaima Lasini

Ni Mwanahabari nchini Morocco. "Nimejifunza kwamba watu husahau unachosema, watu watasahau ulichofanya, lakini watu hawatasahau ulivyowafanya kuhisi-Maya Angelou."

Chiama ni mwanaharakati wa haki za kike, mwanaharakati wa haki za kibinaadamu na mwandishi kutoka mji mkuu wa Rabat ambaye aliongoza maandamano kufuatia unyanyasaji wa msichana mmoja nchini humo

Image caption Mariame Jamme ni mwanzilishi wa shirika la iamth Senegal
  • 7. Mariame Jamme

Ni mwanzilishi wa shirika la iamth Senegal. Elimu ndio funguo ya dunia na pasipoti ya kujipatia uhuru-Oprah Winfrey. Mfanyibiashara huyu na mwanaharakati alijifunza kusoma na kuandika akiwa na umri wa miaka 16 na sasa ni mfanyibiashara wa kibinafsi.

Image caption Nawaal Akram ni mwanamitindo, mcheshi na mwanzilishi wa Muscular Dystrophy nchini Qatar.
  • 8. Nawaal Akram

Ni mwanamitindo, mcheshi na mwanzilishi wa Muscular Dystrophy nchini Qatar. Kwa kawaida huwa na mwangaza mchache katika giza. Nawaal ni mwanaharakati wa watu walemavu na anapigania haki za wanawake walio na ulemavu mashariki ya kati.