Ndoa za kwanza za wapenzi wa jinsia moja zimefanyika Ujerumani

Karl Kreile (kushoto) na Bodo Mende, kutoka Berlin, wameishi pamoja kwa miaka 38 Haki miliki ya picha EPA
Image caption Karl Kreile (kushoto) na Bodo Mende, kutoka Berlin, wameishi pamoja kwa miaka 38

Ndoa za wapenzi wa jinsia moja zimefanyika kwa mara ya kwanza nchini Ujerumani.

Wanaume wawili mjini Berlin ambao wamekuwa pamoja kwa miaka 38 walikuwa wa kwaza kufunga ndoa.

Wapenzi wa jinsia moja nchini Ujerumani wamekuwa wakisajili uhusiano wao tangu mwaka 2001, lakini ni kuanzia tu mwisho wa mwezi Juni ndipo bunge lilipiga kura ya kuwepo usawa wa ndoa.

Kufunga ndoa kutawaruhusu wapenzi wa jinsia moja kunufaika na ulipaji kodi, kupanga watoto kama ndoa za kawaida kati ya mwanamume na mwanamke.

Mada zinazohusiana