Wanawake 100: Wanawake walioshinda tuzo za Nobel wako wapi?

Tuzo ya Nobel Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Medali ya tuzo ya Nobel

Msimu wa Nobel wa 2017 unaendelea huku tuzo za amani , uchumi zikitarajiwa kutangazwa

Lakini katika sayansi , tayari tuzo za mwaka huu zimetangazwa na wengi katika jamii ya wanasayansi wanaona hakuna usawa kuhusu washindi.

Hathaivyo jamii ya wanasaynsi ilibaini kwamba washindi wa tuzo hiyo mwaka huu walikuwa na ulinganifu fulani.

Image caption wanawake 100
  • Je wanawake 100 ni nini?

Makala ya wanawake 100 ya BBC huwataja wanawake 100 walio na ushawishi mkubwa dunia kila mwaka.

Mwaka 2017, tuliwapatia changamoto ya kukabiliana na maswala yanayowakabili wanawake hii leo kama vile ukosefu wa elimu miongoni mwa wanawake, unyanyasaji katika maeneo ya uma na kuwatenga wanawake katika michezo.


Huku tuzo zikitolewa kila mwaka ama hata miongo baada ya kuwatuza ni fursa kwa sherehe kwa makundi yaliohusika.

Mwanaanga, Marytin Rees alisema kwamba wanafizikia watatu waliotuzwa na kamati ya tuzo ya Nobel walikuwa watu imara ambao mchango wao ni tofauti na wa kipekee

Lakini licha ya kufurahishwa na hatua hiyo wanahisi kwamba mabadiliko ni muhimu.

Ni wanawake 17 pekee ambao wametuzwa tuzo za nobel katika orodha tatu za sayansi tangu tuzo hizo zianze mwaka 1909.

Hakujawai kuwa na washindi weusi wa sayansi .

Kati ya washindi 206 wa fizikia waliotambulika, wawili wamekuwa wanawake-Marie Curie[1903] na Maria Goeppert Mayer[1963]

Kuna wanaume wengi wanaoitwa Robert katika orodha ya washindi wa kemia ikilinganishjwa na washindi wa tuzo hilo upande wa wanawake.

Baadhi ya watafiti katika Twitter walilalamikia vigezo vilivyotumika kuwatuza washindi hao.

Kila Tuzo haiwezi kugawanywa na zaidi ya washindi watatu , washindi hawateuliwi na orodha za walioteuliwa huwekwa katika siri kwa miaka 50.

Vera Rubin, Lise Meitner na Jocelyn Bell Burnell walionekana kuwa watu waliokuwa na uwezo wa kushinda tuzo hiyo katika miaka ya nyuma.

Kifo cha Rubin 2016 kinamaanisha kwamba kazi yake kuhusu Mata nyeusi inayodaiwa kuwepo katika eneo kubwa la sayari ya mass sasa ina uwezo wa kutambulika.

Otto Hahn alituzwa tuzo ya nyuklia fishon 1944, ambayo hakuigawanywa , licha ya kuteuliwa katika miaka iliopita na miaka mingine

Burnell na Chien -Shiung Wu ,wote wanafizikia pia waliona taasisi zao zikishinda kwa utafiti walioufanyia kazi lakini hawakushirikishwa.

Ukiangazia umuhimu wa mda mrefu wa kushinda taji la Nobel, tuzo hiyo ni muhimu kwa kupiga jeki kazi yoyote ya utafiti .Mtu anayewania anaweza kupata ufadhili katika sekta ambayo ina ushindani mkubwa kupata ufadhili.

lakini kwa wanawake waliopo katika fizikia na kemia, kuna wachache waliopo kifua mbele. Sekta ya matibabu hatahivyo ina afadhali ikiwa na wanawake 12 walioshinda tuzo hiyo.

Tuzo nyengine kama vile fasihi huwa na usawa wa kijinsia ,huku washinda waliopita akiwemo Alice Munroe, Doris Lessing na Toni Morrison.

Mwaka huu, tuzo hiyo ya fasihi imemwendea mwandishi mwenye asili ya Kijapan na Uingereza kazuo Ishuguro.

Huku harakati za kupigania usawa wa kijinsia zinazopigiwa upato na masharika kama vile Athena Swana na Stemettes zikiendelezwa ,tuzo za Nobel zinasalia kuwa kiwango cha juu zaidi katika ulimwengu wa sayansi.

Ikiwa miongoni mwa chanagmoto za wanawake 100 mwaka huu,kundi moja huko Sillicon valley , ambapo wanawake wana nafasi moja kuu kati ya 10 litaangazia njia za kukabiliana na changomoto hiyo.

Watatoa matokeo yao tarehe sita Ijumaa.

Mada zinazohusiana