Rais Magufuli alifanyia mabadiliko baraza lake la mawaziri Tanzania

Rais Magufuli
Image caption Rais Magufuli

Rais Magufuli ametangaza baraza jipya la mawaziri huku kukiwa na mabadiliko kidogo ambapo amewaondoa mawaziri wanne waliokuemo katika baraza la awali.

Akiwa na takriban miaka miwili ya uongozi amesema amefanya mabadiliko hayo kutokana na kuwepo na nafasi za wazi ambazo zinahitajika kujazwa.

Mawaziri walioachwa ni aliyekuwa Waziri wa Mali asili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe na nafasi yake kuchukuliwa na Hamis Kigwangwala aliyekuwa Naibu Waziri Wizara ya Afya.

Mwingine aliyeachwa ni aliyekuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge ambaye nafasi yake imechukuliwa na Mbunge wa Katavi, Mhandisi Issack Kamwele aliyekuwa naibu waziri wa wizara hiyo.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Annastazia Wambura ambaye nafasi yake imechukuliwa na Mbunge wa Viti Maalum CCM, Juliana Shonza.

Aliyekuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Ramo Makani naye ametupwa nje na nafasi yake kuchukuliwa na Mbunge wa Vwawa, Japhet Hasunga.

Hili ndilo baraza jipya la mawaziri kama lilivyotangazwa na rais Magufuli:

 • 1.Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

I. Waziri - George Huruma Mkuchika

 • 2.Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

I. Waziri - Selemani Said Jafo

II. Naibu Waziri - Joseph Sinkamba Kandege

III. Naibu Wazri - George Joseph Kakunda

 • 3.Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira.

I. Waziri - January Yusuf Makamba

II. Naibu Waziri - Kangi Alphaxard Lugola

 • 4.Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu.

I. Waziri - Jenista Joackim Mhagama

II. Naibu Waziri - Anthony Peter Mavunde (Kazi, Vijana na Ajira)

III. Naibu Waziri - Stella Alex Ikupa (Walemavu)

 • 5.Wizara ya Kilimo.

I. Waziri - Dkt. Charles John Tizeba

II. Naibu Waziri - Dkt. Mary Machuche Mwanjelwa

.6.Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

I. Waziri - Luhaga Joelson Mpina

II. Naibu Waziri - Abdallah Hamis Ulega

 • 7.Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

I. Waziri - Prof. Makame Mbarawa Mnyaa

II. Naibu Waziri - Mhandisi Atashasta Justus Nditiye

III. Naibu Waziri - Elias John Kwandikwa

 • 8.Wizara ya Fedha na Mipango.

I. Waziri - Dkt. Philip Isdor Mpango

II. Naibu Waziri - Dkt. Ashatu Kijaji

 • 9.Wizara ya Nishati.

I. Waziri - Dkt. Medard Matogoro Kalemani

II. Naibu Waziri - Subira Hamis Mgalu

 • 10. Wizara ya Madini.

I. Waziri - Angellah Kairuki

II. Naibu Waziri - Stanslaus Haroon Nyongo

 • 11. Wizara ya Katiba na Sheria.

I. Waziri - Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko

Kabudi.

 • 12. Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

I. Waziri - Dkt. Augustine Philip Mahiga

II. Naibu Waziri - Dkt. Susan Alphonce Kolimba

 • 13. Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga (JKT).

I. Waziri - Dkt. Hussein Ali Mwinyi

 • 14. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

I. Waziri - Mwigulu Lameck Nchemba

II. Naibu Waziri - Mhandisi Hamad Yusuf Masauni

 • 15. Wizara ya Maliasili na Utalii.

I. Waziri - Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla

II. Naibu Waziri - Josephat Ngailonga Hasunga

 • 16. Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

I. Waziri - William Vangimembe Lukuvi

II. Naibu Waziri - Angelina Sylivester Mabula

 • 17. Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.

I. Waziri - Charles Paul Mwijage

II. Naibu Waziri - Mhandisi Stella Martin Manyanya

 • 18. Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi.

I. Waziri - Prof. Joyce Lazaro Ndalichako

II. Naibu Waziri - William Tate Ole Nasha

 • 19. Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

I. Waziri - Ummy Ally Mwalimu

II. Naibu Waziri - Dkt. Faustine Engelbert Ndugulile

 • 20. Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

I. Waziri - Dkt. Harrison George Mwakyembe

II. Naibu Waziri - Juliana Daniel Shonza

 • 21. Wizara ya Maji na Umwagiliaji.

I. Waziri - Mhandisi Isack Aloyce Kamwelwe

II. Naibu Waziri - Jumaa Hamidu Aweso

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Stephen Kagaigai kuwa Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kabla ya Uteuzi huo, Bw. Stephen Kagaigai alikuwa Kaimu Karani wa Baraza la Mawaziri.

Bw. Stephen Kagaigai anachukua nafasi ya Dkt. Thomas D. Kashilila ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Wateule wote wataapishwa Jumatatu tarehe 09 Oktoba, 2017 saa 3:30 Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii