Watafuta ajira kusafiri bila malipo Scotland

scotrail train Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Watafuta ajira kusafiri bila malipo nchini Scotland

Watafuta ajira huko Scotland wanapewa safari za bure kwa njia ya reli katika jitihada za kuondoa moja ya vizuizi vinavyozuia watu kupata ajira.

ScotRail Alliance ilisema kuwa watu wanoatafuta ajira watapata safari mbili za bure kila mwezi za kusafi kwenda kwa maeneo ya kufanyiwa mahojiano ya kazi na kurudi.

Kampuni hiyo pia itatoa safari za bure kwa wale wanaopata ajira kwa mwezi wote wa kwanza wanapopata kazi.

Kampuni hiyo ilisema kuwa msaada huo utasadia kuboresha uchumi wa Scotland.

Mkurugenzi mkuu Alex Hynes alitaja sera hiyo kama moja ya siri zilifichwa zaidi na kampuni yake.

Alisema kuwa gharama ya kusafiri inaweza kuwa kuzuizi kwa watu wanaojaribu kutafuta ajira.

"Msaada tunaotoa kwa watafuta ajira ni moja ya siri kubwa za ScotRail Alliance, lakini ninataka watu wengi zaidi kufahamu kuhusu fursa hii.

Mpango huo unatumiwa tu na wale watu ambao wameandikishwa na kitoa cha kutafuta ajira.

Mada zinazohusiana

Mitandao inayohusiana

BBC haina haihusiki vyovyote na taarifa za mitandao ya kujitegemea