Mwanamume afikishwa mahakamani Dubai kwa kumgusa kwenye kiuno mwanamume mwingine

Jamie Harron Haki miliki ya picha Detained in Dubai
Image caption Jamie Harron amezuiwa kuondoka Dubai

Mwanamume mmoja raia wa Scotland anakabiliwa na kifungo cha miaka 3 mjini Dubai baada ya kugusa kiuno cha manamume mwingine ndani ya baa, amefikiswa mahakamani.

Jamie Harron, kutoka Stirling alifikishwa mahakani leo Jumapili baada ya kuripotiwa kukosa kufika mahakamani awali kwenye mji huo.

Mwanamume huyo wa umri wa miaka 27, alikamatwa kwa kuonyeha tabia mbaya hadharani, kufuatia kisa kwenye baa ya Rock Bottom mjini Dubai tarehe 15 mwezi Julai.

Licha ya hofu kuwa angekamatwa tena, Bw. Harron aliachiliwa lakini akaambiwa kubaki mji humo kuhudhuria mahakama siku za usoni.

Image caption Jamie Harron alikuwa kwenye baa la Rock Bottom

Harron ambaye alikuwa akifaya kazi huko Afghanistan, alisimama mjini Dubai kwa siku mbili wakati kisa hicho kilitokea.

Anasena alikuw anajaribu kuzuia kumwaga kinywaji chake kwenye baa iliyokuwa imejaa watu, kwa akuweka mikono mbele wakati alimguza mwanamume mmoja kimakosa kwenye kiuno kuepeuka kumgonga.

Anaripotiwa kuzuiwa siku tano katika gereza la Al Barsha kabla ya kuachiliwa kwa dhamana ambapo pia alinyanganywa paspoti yake.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii