Mike Pence aondoka uwanjani baada ya wachezaji kupinga ubaguzi

Mike Pence tweeted a photo of himself standing during the US national anthem at an NFL game on Sunday, 8 October 2017

Chanzo cha picha, @VP/Twitter

Maelezo ya picha,

Aliondika baada ya wachezaji wa timu ya San Francisco 49ers haikusimama wakati wa wimbo wa taifa

Makamu wa rais wa Marekani Mike Pence, ameondoka kutoka kwa mechi ya kandanda ya NFL nchini Marekani, baada wachezaji kukataa kusimama wakati wa kuchezwa kwa wimbo wa taifa wa Marekani.

Bw. Pence alisema kuwa hatakuwa kwenye warsha ambayo haiheshimu wanajeshi wa Marekani au bendera baada ya kuondoka kwenye mechi iliyokuwa ikichezwa katika jimbo nyumbani kwake huko Indiana.

Rais Donald Trump aliandika katika mtandao wa twitter kuwa alimuomba Pence kuondoka ikiwa wachezaji wangepiga magoti.

Kupiga magoti wakati wa mechi za NFL imekuwa njia ya kupinga ubaguzi wa rangi.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mike Pence aliondika baada ya wachezaji wa timu ya San Francisco 49ers haikusimama wakati wa wimbo wa taifa

Trump amewakosoa wachezaji vikali na kuitaka NFL kuwapiga marufuku.

"Niliondoka katika mechi ya leo kwa sababu rais Trump na mimi hatutakubali warsha yoyote ambayo haieshimu wanajeshi wetu, bendera yetu au wimbo wetu wa taifa," Pence aliandika kwenye twitter siku ya Jumapili.

Aliondoka baada ya wachezaji wa timu ya San Francisco 49ers haikusimama wakati wa wimbo wa taifa kabla ya mechi dhidi ya Indianapolis Colts.

Awali Bw. Trump alisema kuwa matamshi yake ya kukosoa hatua za NFL hayakuhusu kwa vyoyote vile suala la rangi.