Hamas na Fatah waingia katika mkataba

Viongozi wa Palestina katika mkutano wa awali
Image caption Viongozi wa Palestina katika mkutano wa awali

Msemaji wa kundi la wapiganaji wa Palestina ,Hamas amesema kuwa kundi hilo limeafikiana na kundi pinzani la Fatah kusitisha mzozo wa muongo mmoja kati yao.

Msemaji huyo amesema kuwa maelezo ya makubaliano hayo yatatangazwa katika mkutano na vyombo vya habari mjini Cairo, ambapo awamu ya pili ya mazungumzo ya upatanishi yanaanza siku ya Jumanne.

Hakujakuwa na ithibati yoyote kutoka kwa Fatah.

Mwezi uliopita Hamas lilisema litafutilia mbali kamati ambayo ilisimamia eneo la Gaza na kutoa udhibiti wake kwa serikali inayoungwa mkono na Fatah katika ukanda wa West Bank.

Image caption Ramani ya Palestina

Hamas lilichukua udhibti wa Gaza baada ya kuliondoa kwa nguvu kundi la wapiganaji wa Fatah 2007.- mwaka baada ya Hamas kushinda uchanguzi wa Palestina.

Mada zinazohusiana