Pakistan yaokoa familia iliyotekwa na Taliban miaka 5 iliyopita

Pakistani soldiers (file photo) Haki miliki ya picha AFP
Image caption Pakistan yaokoa familia iliyotekwa na Taliban miaka 5 iliyopita

Jeshi la Pakistan limeiokoa familia moja ya watu watano raia wa Marekani ambao walikuwa wakishikwa mateka na wanamgambo wa Taliban wa Afghanistan.

Waliokolewa wakati wa oparesheni katika wilaya moja yenye makabila ya Kurram karibu na mpaka na Afghanistan.

Jeshi la Afghanistan halikuitaja familia hiyo, lakini raia wa Canada Joshua Boyle na mkewe raia wa Marekani Caitlan Coleman, walitekwa walipokuwa wakitembea nchini Afghanistan mwaka 2012.

Wanaaminika kupata watoto wakiwa mateka.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Pakistan yaokoa familia iliyotekwa na Taliban miaka 5 iliyopita

Video ya mwisho ya wawili hao ilitolewa Disemba mwaka uliopita wakati walionekana wakiomba nchi zao kuwaokoa.

Walionekana wakiwashika watoto wao wadogo wa kiume waliozaliwa wakiwa wameshikwa mateka.

Haikujulikana ni lini video hiyo ilirekodiwa, lakini ilitolewa baada ya uvumi kusambaa mjini Kabul kuwa serikali ilikuwa ikipanga kumnyonga Anas Haqqani, mtoto wa mwanzilishi wa mtandoa wa Haqqani ambaye amekuwa akizuiliwa tangu mwaka 2014.

Mada zinazohusiana