Kenya: Hakuna msamaha kwa watakaopatikana na mifuko ya plastiki

Watakoshikwa tena na mifuko ya plastiki watafungwa kifungo cha miaka minne gerezani au faini ya dola 40,000 Haki miliki ya picha SIMON MAINA/AFP/GETTY IMAGES
Image caption Watakoshikwa tena na mifuko ya plastiki watafungwa kifungo cha miaka minne gerezani au faini ya dola 40,000

Mahakama nchini Kenya imewaachilia watu 11 na onyo kali, baada ya kukukubali mashtaka ya kukiuka sheria mpya ya Mazingira , ambayo imepiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki iliyo na adhabu kali zaidi duniani.

Washukiwa hao kumi na mmoja walinaswa kwenye operesheni iliyofanywa na Mamlaka ya Kusimamia Ubora wa Mazingira nchini Kenya na kushtakiwa kwa kuuza miwa iliyofungwakwa mifuko ya plastiki, iliyopigwa marufuku katika barabara za mji wa Mombasa.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Takataka ya plastiki huwa shida kubwa kwa Mazingira katika nchi nyingi barani Afrika

Walikiri mashtaka lakini wakaomba msamaha kwa kuwa hii ilikuwa hatia yao ya kwanza.

Upande wa mashtaka ulitaka watumiwe kama mfano kwa wale wanaopuuza sheria hiyo, lakini hakimu Martin Rabera aliwaachilia baada ya kuwapa onyo kali na kuamrisha operesheni hiyo iendelee.

Sheria mpya ya mazingira nchini Kenya imepiga marufuku kutengeneza, kuuza au hata kutumia mifuko ya plastiki huku adhabu yake ikiwa kifungo cha miaka minne gerezani au faini ya dola 40,000.

Image caption Ng'ombe wanaokula taka nchini Kenya hupatikana na mifuko ya plastiki tumboni

Kabla ya marufuku hiyo kuanza kutekelezwa mwishoni mwa mwezi Agosti, mifuko ya plastiki ilitumika sana kubeba mizigo nchini Kenya.

Lakini wanasayansi walionya kwamba plastiki ilikuwa inaharibu mazingira, inaua wanyama wanaoila mifuko hiyo na pia sumu yake huingia katika miili ya binadamu kwa kula nyama ya mifugo walioila mifuko hiyo.

Mada zinazohusiana