Ndege ya Uturuki yatua kwa dharura pwani ya Kenya

Ndege ya Uturuki yatua kwa ghafla katika uwanja wa ndege wa Moi mjini Mombasa Kenya
Image caption Ndege ya Uturuki yatua kwa ghafla katika uwanja wa ndege wa Moi mjini Mombasa Kenya

Ndege moja ya kampuni ya ndege ya Uturuki Turkish Airlines iliokuwa ikibeba abiria 121 na wafanyikazi sita ilitua kwa dharura nchini Kenya siku ya Ijumaa alfajiri baada ya mojawapo ya injini zake kuingiwa na ndege, kulingana na polisi.

Ndege hiyo aina ya TK673 ilikuwa ikiondoka katika mji huo wa pwani ya Kenya ikielekea Istanbul wakati ndege huyo alipoingia katika injini yake mwendo wa saa 10 alfajiri .

Ilibidi ndege hiyo izunguke katika anga ya mombasa kwa takriban saa moja ili kumaliza mafuta yake kabla ya kutua kwa dharura.

Hakuna mtu aliyejeruhiwa.

Ndege hiyo ilichunguzwa na mafundi kabla ya kuondoka.

Mada zinazohusiana