Afrika: Picha za kutoka 6-12 Oktoba 2017

Baadhi ya picha zilizovutia zaidi kutoka barani Afrika na za Waafrika walioko sehemu mbali mbali duniani wiki hii.

Watoto wa kisomali wanaogelea na kucheza mbele ya magofu ya nyumba ya zamani katika pwani ya Hamarweyne, jijini Mogadishu Ijumaa. Haki miliki ya picha AFP

Vijana wa Kisomali wakifurahia Ijumaa kwa kupiga mbizi, kucheza na kuogelea mbele ya magofu ya nyumba ya zamani katika pwani ya Hamarweyne, jijini Mogadishu

A man in a traditional costume performs ahead of the Rugby test match between South Africa (Springboks) and New Zealand (All Blacks) at Newlands Rugby stadium on October 7, 2017 in Cape Town. / AF Haki miliki ya picha AFP

Nchini Afrika Kusini, Mwanaume aliyevalia mavazi za kitamaduni wanatumbiza watu kabla ya mchuano wa majaribio wa raga kati ya Springboks na All Blacks mjini Cape Town.

Picha iliyopigwa tarehe 8 Oktoba, 2017 jijini Accra yaonyesha gari zilizochomeka mahala ambapo lori ya gesi ilishika moto, na kusababisha milipuko katika stesheni mbili za mafuta jioni ya tarehe 7 Oktoba. Watu watatu walifariki na wengine wengi kujeruhia Haki miliki ya picha AFP

Masalio ya mkasa wa moto Jumamosi baada ya lori lililokuwa likibeba gesi kushika moto katika mji mkuu wa Ghana, Accra, na kusababisha mlipuko mkubwa.

Wanamitindo wanaonyesha mavazi yaliyotengenezwa na mbunifu wa manguo Bi Zahui wakati wa maonyesho ya mavazi ya Afrik mjini Abidjan 07/10/2017 Haki miliki ya picha EPA

Wanamitindo wanaonyesha mavazi yaliyotengenezwa na mbunifu wa nguo Bi Zahui wakati wa maonyesho ya mavazi ya Afrik mjini Abidjan siku ya Jumamosi.

Mwanamitindo anaonyesha mavazi yaliyotengenezwa na mbunifu Nadir Tati siku ya Jumapili wakati wa maonyesho ya mavazi ya Lisbon Haki miliki ya picha EPA

Bara jingine, maonyesho mengine. Raundi hii ikifanyika mjini Lisbon, ambako mavazi ya mbunifu kutoka Angola Nadir Tati yalionyeshwa katika wiki ya kuonyesha mavazi Jumapili.

Wanawake wanatazama Misri ikichuana na Congo katika mashindano ya mchujo ya kandanda katika uwanja wa mpira, mjini Alexandria, Egypt - 08/10/2018 Haki miliki ya picha Reuters

Mechi ya kandanda ya kufuzu kwa Kombe la dunia 2018 kati ya Misri na Congo Brazzaville iliwavutia mashabiki wengi katika uwanja wa mpira wa Borg El Arab Stadium mjini Alexandria siku ya Jumapili.

Wanaume kutoka Misri watizama timu yao ya nyumbani ikichuana na timu kutoka Congo Brazzaville katika runinga pana Haki miliki ya picha EPA

Furaha kwa Wamisri, timu yao ilishinda 2-1, na kupata nafasi ya kucheza katika fainali hizo za Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya miongo miwili.

Mohamed el-Morabity kutoka Morocco, anajimwagilia maji usoni alipokuwa anakimbia na kushinda mbio za marathon za El Djerid katika nyikakatika mji wa Tozeur. Haki miliki ya picha AFP

Wakimbiaji wengine walikimbia wikendi katika mbio za nyika za kilomita 100 nchini Tunisia.

Mohamed el-Morabity mzaliwa wa nchi ya Morocco ambaye alishinda mbio hizo anaonekana hapa akikata kiu.

Wafuasi wa chama cha Coalition for Democratic Change inayoongozwa na Georgia Weah, wanasikiza matokeo ya urais wa Liberia katika redio. Haki miliki ya picha EPA

Siku moja baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika Jumanne nchini Liberia, wafuasi wa chama cha Coalition for Democratic Change kinachoongozwa na Georgia Weah wanafuatilia matukio katika redio kujua rais wao mpya ni nani.

Polisi wa kupambana na ghasia wanasimama kidete huku wafuasi wa mrengo wa upinzani National Super Alliance (NASA) wakifanya maandamano jijini Nairobi, Kenya 11/10/2017 Haki miliki ya picha Reuters

Polisi wa kupambana na ghasia wakisimama kidete huku wafuasi wa mrengo wa upinzani National Super Alliance (NASA) wakifanya maandamano jijini Nairobi, Kenya siku ya Jumatano.

Wafuasi wa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wanatawanyishwa katika mtaa mmoja jijini Nairobi, Kenya 11/10/2017 Haki miliki ya picha Reuters

... na hapa polisi wanawatawanya wafuasi wa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta waliojitokeza kuwakabili wafuasi wa Bw Raila Odinga.

Mwanaume anapita mbele ya mchoro mkubwa inayoonyesha ndovu jijini Johannesburg, South Afrika, Oktoba 10, 2017. Haki miliki ya picha EPA

Mchoro mkubwa katikati mwa mji wa Johannesburg uliochorwa na mchoraji wa grafiti "Falko", sasa ni mmojawepo ya vivutio vya utalii vinayoonyesha mandhari ya mji huo.

wanadensi wa Ballet kutoka mjini Joburg wanajiandaa kwa maonyesho ya mwisho ya Snow White nchini Afrika Kusini 12 October 2017. Haki miliki ya picha EPA

Tukisalia na sanaa wacheza dansi ya Ballet kutoka mjini Jo'burg wanajiandaa kwa maonyesho ya mwisho ya Snow White nchini Afrika Kusini 12 October 2017.

Picha kwa hisani ya AFP, EPA, PA na Reuters

Mada zinazohusiana