Murkomen: Marekebisho ya sheria za uchaguzi yataifaa Kenya
Huwezi kusikiliza tena

Murkomen: Marekebisho ya sheria za uchaguzi yataifaa Kenya

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amepokea mswada tata wa kufanyia marekebisho sheria za uchaguzi kutoka bunge la Senate na kuahidi kuudurusu mswada huo kabla ya kutia saini au kuurejesha kwa Bunge katika kipindi cha siku kumi na nne.

Mswada huo tata ulipitishwa katika mabunge yote mawili licha ya shinikizo kutoka jamii ya kimataifa kutaka zisitekelezwe wakati huu wakati kuna msukosuko nchini humo.

Je Mbona chama tawala cha Jubilee kimeshinikiza kupitishwa kwa sheria hiyo wakati huu.

Kiongozi wa wengi katika bunge la Seneti Kipchumba Murkomen amezungumza na BBC.

Mada zinazohusiana