Diane Rwigara amwomba Rais Kagame afueni

Rwanda Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Diane Rwigara kiongozi wa upinzani nchini Rwanda

Kiongozi wa upinzani nchini Rwanda Diane Rwigara amemwomba Rais Paul Kagame kumuachilia yeye, mamake na dadake.

Akiwa mahakamani, Bi Rwigara amesema kwamba serikali imefanya jaribio la kuinyamazisha familia yake pamoja na wafuasi wake tangu alipotangaza kuwania nafasi ya uraisi katika uchaguzi uliofanyika mwezi May mwaka huu.

Wawake hao watatu, ambao walikamtwa mwezi uliopita, wameshtakiwa kwa makosa ya udanganyifu na uchochezi tuhuma ambazo wameziita zenye mrengo wa kisiasa.

Bi Rwigara alizuiliwa kuendelea na nia yake ya kunwania nafasi ya uraisi wa Rwanda, Uchaguzi ambao Bwana Kagame alishinda kwa kishindo kwa karibu asilimia tisini na tisa ya kura zote zilizopigwa.