Viongozi wa Catalonia wazuiwa rumande Uhispania

Jordi Cuixart (L), leader of Omnium Cultural, and Jordi Sanchez of the Catalan National Assembly (ANC), arrive to the High Court in Madrid, Spain, October 16, 2017 Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Viongozi wa Catalonia wazuiwa rumande Uhispania

Jaji nchini Uhispania amewazuia rumande wanachama wakuu wa harakati za uhuru wa Catalonia.

Jordi Sánchez, ambaye anaongoza bunge la Catalonia na Jordi Cuixart, kiongozi wa vuguvugu la Omnium Cultural, wanazuiwa huku wakifanyiwa uchunguzi wa uhaini.

Wanaume hao wanaonekaka kama viongozi wakuu wa kupanga kura ya uhuru wa tarehe 1 Oktoba ambayo ulifutwa na mahakama ya Uhispania.

Serikali nchini Uhispania ilitangaza kura hiyo kuwa iliyo kinyume na sheria.

Kufuatia kura hiyo kiongozi wa eneo la Catalonia Carles Puigdemont, alisaini hatua ya kutangaza uhuru lakini akazuia kutekeleza tangazo hilo.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Watu wanaounga mkono uhuru wa Catalonia mjini Barcelona

Ametaka mazungumzo kufanyika ndani ya miezi miwili inayokuja.

Hata hivyo serikali ya Uhispania imeonya kuwa Catalonia ni lazima ifute tangazo hilo au ikabiliwe na uongozi wa moja kwa moja kutoka Madrid.

Bw. Puigdemont pia ameikasirisha Madrid kwa kukataa kuthibitisha ikiwa ametangaza uhuru au la wiki iliyopita.

Bw. Puigdemont ambaye amepewa hadi Alhamisi kutangaza msimamo wake, aliishambulia serikali katika mtandao wa Twitter kufuatia habari za kuzuiwa kwa Bw. Sánchez na Bw. Cuixart's

Mada zinazohusiana