Rais Zuma amfuta kazi waziri wa elimu ya juu

Rais Zuma amfuta kazi waziri wa elimu ya juu Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais Zuma amfuta kazi waziri wa elimu ya juu

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, amemfuta kazi mkosoaji wake mkubwa kutoka kwa serikali yake.

Kiongozi wa chama cha Communist Blade Nzimande, ambaye amekosoa ufisadi mkubwa ndani ya serikali na kuunga mkono kampeni za urais za mfanya biashara tajiri Cyril Ramaphosa, alifutwa kutoka wizara ya elimu ya juu.

Katika mabadiliko mengine Bw. Zuma pia alimteua waziri wa usalama wa nchi David Mahlolo, kuwa waziri wa nishati.

Mabadiliko hayo yanakuja wakati bunge la Afrika Kusini linaanzisha uchunguzi unaohusu madai ya ufisadi wa kiwango cha juu zaidi serikalini.

Wale waliopiga ramli kuhusu ufisadi huo na maafisa mashuhuri wanatarajiwa kuitwa kutoa ushahidi wao.

Mada zinazohusiana