Upinzani waahirisha maandamano yake Kenya

Upinzani nchini Kenya NASA Jumanne uliahirisha maandamano yake dhidi ya tume ya uchaguzi nchini humo IEBC
Image caption Upinzani nchini Kenya NASA Jumanne uliahirisha maandamano yake dhidi ya tume ya uchaguzi nchini humo IEBC

Upinzani nchini Kenya NASA Jumanne uliahirisha maandamano yake dhidi ya tume ya uchaguzi nchini humo IEBC huku kukiwa na madai ya maafisa wa polisi kutumia nguvu zaidi dhidi ya waandamanaji.

Kiongozi wa upinzani nchini humo Raila Odinga amesema kuwa muungano huo utatoa mwelekeo wake baada ya siku ya Mashujaa itakayofanyika Ijumaa .

Hatua hiyo , Odinga amesema imeafikiwa kufuatia vifo vya baadhi ya wafuasi wake ambao alidai walipigwa risasi na polisi.

Taarifa ya Odinga pia ilimlaumu waziri wa usalama Fred Matiangi na inspekta jenerali wa polisi Joseph Boinet akiwashutumu kwa kuwaagiza maafisa wa polisi kuwa raia wasio na hatia.

Kwa heshima ya wale waliouawa na serikali, maandamano yetu yataahirishwa.

''Siku ya Ijumaa tutawakumbuka raia wasio na hatia kama mashujaa kwa harakati dhidi ya haki ya uchaguzi katika eneo ambalo tutalitaja baadaye.Siku hiyo tutatangaza hatua tutakayochukua'', alisema kiongozi huyo wa upinzani.

Image caption Wafuasi wa NASA wakifanya maandamano dhidi ya tume ya uchaguzi nchini humo IEBC

Nasa, imesema inawataka maafisa wa polisi kukomesha mauaji hayo ambayo amesema kuwa ni gharama kubwa kwa taifa.

''Serikali lazima isitishe ushirikiano wa maafisa wa polisi na majambazi mbali na ukiukaji wa kikatiba wa kuwapeleka polisi kuwakabili wafuasi wa NASA'', alisema.

Mapema siku ya Jumanne , Mahakama kuu ilisitisha kwa muda marufuku ya serikali dhidi ya maandamano ya IEBC katikati mwa miji ya Nairibi, Mombasa na Kisumu.

Hatua hiyo inajiri kufuatia kesi iliowasilishwa na afisa mkuu mtendaji wa NASA Norman Magaya.

Mada zinazohusiana