Tanzania kuwapiga mnada zaidi ya ng'ombe 1000 kutoka Kenya
Huwezi kusikiliza tena

Tanzania kuwapiga mnada zaidi ya ng'ombe 1000 kutoka Kenya

Tanzania imesema ipo katika hatua za mwisho za maandalizi ya kupiga mnada ng'ombe zaidi ya 1,000 waliokamatwa kaskazini mwa Tanzania mkoani Kilimanjaro walioingia nchini humo kutoka Kenya.

Hayo yamesemwa na waziri wa mifugo wa Tanzania Luhaga Mpina ambaye ameongeza kuwa operesheni dhidi ya mifugo kutoka nchi jirani itaendelea katika mipaka yote.

Awali Mwandishi wa BBC Leonard Mubali alifanya mahojiano kwa njia ya simu na waziri huyo ambaye yupo mkoani humo akisimamia maandalizi ya kuuzwa kwa ng'ombe hao na anaanza kuelezea hatua waliofikia kuwauza.