Mtoto aliyepigwa risasi kwenye maandamano Kenya atolewa risasi hiyo

Image caption Mtoto aliyepigwa risasi kwenye maandamano Kenya atolewa risasi hiyo

Madaktari wameondoa risasi kutoka wa bega la mtoto wa umri wa miaka miwili unusu, ambaye alipigwa risasi wakati wa maandamano ya kutaka mabadiliko kufanyiwa tume ya uchaguzi kwenye mji wa magharibi mwa Kenya Kisumu.

Lydia Khageya, mamake mtoto huyo aliliambia gazeti la Star la nchini humo kuwa mtot hiyo, alipigwa risasi wakati akicheza na watoto wengine nyumbani kwao.

"Tulikimbia kweda eneo alikuwa kwa sabbabu tulidhani kuwa alikuwa amegongwa na jiwe, lakini tulipoangalia kwa makini tukaona kitu kwenye bega lake ndipo tukampeleka hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga," alisema mama yake.

Hii leo mahakama kuu nchini kenya imeondoa kwa muda marufuku kwa maandamano dhidi ya tume ya uchaguzi ya chi hiyo IEBC.

Muungano wa upinzani (Nasa) ulikuwa tayari umetangaza kuwa haungefanya maandamano leo dhidi ya tume ya uchaguzi, ili kuwaruhusu viongozi wake kuwatembelea watu walipigwa na polisi wakati wa maandamano.