Mji wa Raqqa nchini Syria wakombolewa

Syria Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mji wa Raqqa uliokombolewa

Bendera ya wanamgambo wa kupambana na kundi la wanamgambo wenye msimamo mkali la I-S imekuwa ikipepea juu ya mji wa Raqqa, baada ya kuuweka mji huo wa Syria katika himaya yake baada ya mapambano ya nguvu ya miezi minne mfululizo.

Wanamgambo hao wenye asili ya Kurdi na Uarabuni wametoa tamko la kwamba sasa wanaudhibiti mji wa Raqqa, lakini wasaidizi wao Marekani wameonya kuwa wapiganaji hao wa Kiislam wanaokadiriwa kufikia mia moja wanaishi katika mji huo na kwamba Marekani imesema kwamba iko tayari kutoa usaidizi wowote utakao hitajika.

Tatizo lingine kubwa lililopo kwa sasa ni ukusanyaji na uondoaji wa mabomu yaliyosimikwa kwatika makazi ya watu na kwenye mji wote wa Raqqa.

Waangalizi wa masuala ya kimataifa wamearifu kuwa zaidi ya watu elfu tatu wameuawa katika kipindi cha mapambano ya kuukomboa mji huo, na miongoni mwao theluthi moja ni raia.