Tuhuma za ngono kwenye filamu zazua balaa

Marekani Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption wacheza filamu walioingia kwenye mzozo wa tuhuma za ngono , kushoto ni Harvey Weinstein na Rose McGowan wakiwa pamoja mwaka 2007

Mkuu wa studio ya kurekodia ya Amazon, Roy Price,ameamua kujiuzulu baada ya taarifa za kumnyanyasa mzalishaji mziki na kutupilia mbali shutuma za unyanyasaji wa kingono dhidi yake zilizotolewa juu ya mcheza filamu nguli Harvey Weinstein.

Kujiuzulu kwake kunafuatia ujumbe mfululizo kwenye mtandao wa kijamii uliokuwa ukitumwa na muigizaji mwenye asili ya Marekani Rose McGowan ujumbe huo ukielekezwa zaidi kwa mkuu wa Amazon, Jeff Bezos.

Katika moja ya ujumbe huo anasema Bw Price alikuwa amepuuza mara kwa mara malalamiko yake ya ubakaji aliotendewa na bwana Weinstein.

Mzalishaji huyo wa muziki amekana tuhuma zote za kudai kuwa kulikuwa na kitendo cha ngono isiyo ya kujamiiana. Mpaka sasa hakuna maoni kutoka kwa mtuhumiwa bwana Price.