Mahakama nchini Marekani yamgomea Trump

Wahamiaji Marekani kutoka nchi za Kiislamu Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption Wahamiaji Marekani kutoka nchi za Kiislamu

Majaji nchini Marekani wamezuia toleo jipya la marufuku ya kusafiri la Rais Donald Trump, saa kadhaa kabla halijaanza kutekelezwa.

Jaji katika mahakama ya Hawaii, Derrick Watson amesema marufuku hiyo imekuwa na dosari zinazofanana na marufuku ya mwanzo katika toleo la awali, ambayo inavunja sheria za uhamiaji za Marekani. Na hazioneshi raia kutoka nchi sita za Kiislamu, Korea kaskazini na maafisa wa Venezuela ambao ni kitisho kwa Marekani.

Ikulu ya Marekani imeuita uamuzi huo wa mahakama kama wenye mapungufu, huku Wizara ya sheria ya nchi hiyo ikisema kwamba itakata rufaa kupinga uamuzi huo.