Liverpool yapata ushindi wa 7-0 dhidi ya NK Maribor

Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp amesema kuwa ni vyema kuweka historia huku kikosi chake kikiivuruga klabu ya Slovenia Marobor
Image caption Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp amesema kuwa ni vyema kuweka historia huku kikosi chake kikiivuruga klabu ya Slovenia Marobor

Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp amesema kuwa ni vyema kuweka historia huku kikosi chake kikiivuruga klabu ya Slovenia Marobor na kupata ushindi mkubwa wa klabu ya Uingereza katika historia ya kombe la Ulaya.

Liverpool ilitawala mechi yote na kuweza kupanda katika kilele cha kundi E kwa kuonyesha mchezo mzuri.

Roberto Firmino na Mohammed Salah wote walifunga mara mbili, huku Phillipe Coutinho , Alex Oxlaide Chamberlain na Trnt Alexander Arnold pia wakicheka na wavu.

Ushindi huo unaupiku uliwe wa 6-0 wa Leeds dhidi ya klabu ya Norway ya Lyn mnamo mwezi Oktoba 1969 na ule wa Manchester United dhidi ya klabu ya Ireland ya Shamrock Rovers mnamo mwezi Septemba 1957.

''Niliambiwa kuhusu rekodi hiyo baada ya mechi lakini sikujua'', alisema Klopp.

Mada zinazohusiana