Watu wanne wauawa katika maandamano dhidi ya serikali Togo

Waandamanaji Togo Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waandamanaji Togo

Watu wanne wameuawa katika maandamano ya kuipinga serikali nchini Togo.

Waandamanaji walipambana na wanajeshi katika mji mkuu wa Lome na mji wa pili kwa ukubwa wa Sokode kwa kuweka vizuizi na kufunga barabara.

Polisi na wanajeshi walifyatua mabomu ya kutoa machozi kujaribu kuwatawanya watu hao.

Vifo hivyo vimetokea katika kampeni ya hivi karibuni kuzuia jaribio la Rais wa nchi hiyo Faure Gnassingbe, kubadili katiba ya nchi hiyo.

Waandamanaji hao wanataka Rais hyo aondoke madarakani muda wake utakapoisha 2020 na kutokaa tena uongozini kwa awamu mbili.

Mada zinazohusiana