Theresa May atoa ahadi kwa raia wa EU

Waziri mkuu wa Uingereza amekuwa akisema kuwa Mstakabali wa raia wa Ulaya, ndio kipaumbele chake
Maelezo ya picha,

Waziri mkuu wa Uingereza amekuwa akisema kuwa Mstakabali wa raia wa Ulaya, ndio kipaumbele chake

Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May ametoa ahadi mpya kwa raia wa Ulaya kwamba itakuwa rahisi iwezekanavyo kuendelea kuishi Uingereza baada ya nchi hiyo kujiondoa katika Umoja wa Ulaya.

Ametoa kauli hiyo katika barua ya wazi iliyoitanguliza, atakapo wahutubia viongozi wenzake wa serikali wa Umoja wa Ulaya mjini Brussels Ubelgiji.

Habari zinasema kuwa viongozi hawatakubali kufanya mazungumzo ya kibiashara na Uingereza katika mkutano wao wa leo lakini wanaweza kufanya hivyo wakati watakapokutana pamoja mwezi Desemba.

Akizungumzia mkutano huo, kwa upande wake Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya Donald Tusk amesema hakutakuwa na mpenyo katika mkutano huo wa siku mbili, lakini mafanikio yanaweza kuonekana katika mkutano mwingine wa viongozi wa Ulaya uliopanga kufanyika Desemba.