Nyiragongo: Mlima wa kipekee mashariki mwa DR Congo

Nyiragongo: Mlima wa kipekee mashariki mwa DR Congo

Jamuhuri ya kidmokrasia ya Congo ni mojawapo ya nchi zenye vivutio vingi na vya aina yake duniani. Moja kati ya vivutio hivyo ni hifadhi ya wanyama ya Virunga, ambayo humo ndani kunapatikana milima ya volkano ya Nyiragongo.

Tangu mwaka wa 2002, hifadhi hiyo ilitelekezwa kutokana na hali ya kisiasa na vurugu za mara kwa mara. Mwandishi wa BBC wa maeneo ya mashariki mwa Congo Byobe Malenga ametembelea eneo hilo.