Hoteli kubwa ya kifahari yateketea moto Myanmar

A firefighter extinguishes a fire at Kandawgyi Palace hotel in Yangon early on 19 October 2017 Haki miliki ya picha AFP/Getty Images
Image caption Moto huo ulianza mapema Alhamisi

Moto mkubwa imeteketeza hoteli kubwa ya kifahari katika mji wa Yangon nchini Myanmar na kumuua mtu mmoja.

Watu wengine walijeruhiwa kwenye moto huo ambao ulianza mwendo wa saa 20:30 GMT siku ya Jumatano katika hoteli ya Kandawgyi Palace.

Hoteli hiyo ilikuwa maarufu wa watalii.

Haki miliki ya picha AFP/Getty Images
Image caption Moto mkubwa uliwaka

Iliwachukua mamia ya wazima moto saa kadha kuuzima moto huo. Zaidi ya wageni 140 waliondolewa.

Haijuliana moto huo ulinza kwa njia gani huku ripoti za kukanganya zikisema kuwa kulikuwa na mlipuko wa mtungi wa gesi au hutilafu ya umeme.

Haki miliki ya picha AFP/Getty Images
Image caption Mamia ya wazima walitumwa kuuzima moto huo

"Hakukuwa na king'ora na vurugu zilikuwa ni kama kulikuwa na walevi hotelini," mtalii mmoja alisema, akiongeza kuwa ni mfanyakazi mmoja ambaye alimuelekzea eneo salama.

Wageni wamehamishwa kweda kwa hoteli zingine mjiji Yangon.

Haki miliki ya picha Alamy
Image caption Hoteli ya kifahari kabla ya kuteketea
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Moshi bado ulikuwa ukitoka kwenye mabaki ya hoteli hiyo

Hoteli hiyo ili kando ya ziwa Kandawgyi, ilijengwa miaka ya 1990 lakini huenda uwepo wake uliazia miaka ya 1930 wakati eneo hilo lilikuwa likitumia kama klabu ya wanajeshi wa Uingereza.

Mada zinazohusiana