Uchafuzi wasababisha % 16 ya vifo

Uchafuzi ndio chanzo cha asilimia 16 ya vifo duniani Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Uchafuzi ndio chanzo cha asilimia 16 ya vifo duniani

Utafiti wa kimataifa uliofanywa umekadiria kwamba uchafu ndio chanzo cha vifo vya watu milioni tisa duniani kote katika kipindi cha mwaka 2015.

Utafiti uliochapishwa katika jarida la Lancet umechanganua taarifa za dunia kuhusiana na magonjwa yaliyosababishwa na uchafu wa mazingira kama vile magonjwa ya moyo na magonjwa ya kupooza.

Vifo hivyo vya mapema vinaelezwa kuweka asilimia 16 ya vifo duniani kote.

Uchafuzi wa anga ndio sababu kubwa, ikifuatiwa na uchafuzi wa maji.

Utafiti huo unaonesha kuwa karibu asilimia kubwa ya vifo hivyo vinavyotokana na uchafuzi vimetokea katika nchi zenye kipato cha chini na kati.