Lupita Nyong'o adai kunyanyaswa kijinsia na Weinstein

Lupita ni miongoni mwa wanawake wanaodai kunyanyaswa na Weinstein
Image caption Lupita ni miongoni mwa wanawake wanaodai kunyanyaswa na Weinstein

Nyota wa Hollywood kutoka Kenya Lupita Nyong'o ndiye mwanamke wa hivi karibuni kumshutumu mtayarishaji filamu Harvey Weinstein kwa unyanyasaji wa kijinsia akitoa msururu wa taarifa kuhusu vile jamaa huyo alivyotaka kumsaidia kuimarisha kazi yake iwapo wangefanya naye ngono.

Kwa mujibu wa kituo cha habari cha AFP mshindi huyo wa tuzo ya Oscar katika filamu ya 12 Years a Slave' alielezea njia kadhaa alizochukua bwana Weinstein akijaribu kumtongoza wakati alipokuwa mwanafunzi katika chuo cha uigizaji cha Yale.

Lupita anasema kuwa walikutana na mtayarishaji huyo wa filamu 2011 katika tamasha la filamu na alimualika katika nyumba yake ili kutazama filamu aliyokuwa ameitayarisha.

Dakika 15 baada ya filamu hiyo kuanza , bwana Weinstein , na mwanawe mdogo wakiwa katika nyumba yao wakati huo, alimpeleka katika eneo jingine la nyumba hiyo.

''Harvey alinipeleka hadi katika chumba chake cha kulala na kumwambia kwamba angependa kumfanyia masaji'', Lupita aliandika.

Nilidhani anafanya mzaha mara ya kwanza, Lupita aliendelea. Hakuwa akifanya mzaha.Tangu mara ya kwanza nilipokutana naye nilijihisi sina usalama wa kutosha.

Nilikuwa na wasiwasi na nikaomba nimfanyie masaji hiyo yeye badale yake.

Nilijaribu kudhibiti hali ili kujua pale mikono yake ilipokuwa kila mara.

Image caption Mtayarishaji wa filamu Harvey Weinstein

Aliongezea: Nilianza kumfanyia masaji mgongo wake ili kupata muda wa kufirikia nitakavyojiondoa katika hali hiyo.

Na baada ya muda mfupi alisema kuwa anataka kuvua suruali yake ndefu.

Nilimwambia asifanye hivyo na nikamwalezea kwamba sitahisi vyema kuwa naye.

Kisa hicho kilikwisha na akaondoka kuelekea nyumbani.

Lupita alikiri kwamba ''sikujua vile nitakavyokabiliana na kisa hicho cha masaji'', aliongezea.

Lakini nilijua kwamba sitokubali tena kuzuru maeneo ya kibinafsi na Harvey Weinstein.

Lakini bwana Weinstein alisisitiza kuniona.

Bwana Weinstein alinialika katika filamu moja mjini New York .Alijiunga naye katika mgahawa mmoja akitumai kwamba kutakuwa na watu wengine.

Badala yake alikuwa pekee.

Aliniambia nina chumba cha kibinafsi katika gorofa ya juu ambapo tunaweza kupumzika na kumaliza chakula chetu .Nilishangaa.

Nilimwambia ninapendelea kula katika mgahawa.Wacha kujifanya huelewi mambo, liniambia.

Iwapo ningetaka kuwa mwigizaji maarufu wa filamu basi sina budi bali kujihusisha na tendo hilo.

Alisema alikuwa na uhusiano na waigizaji maarufu X na Y na tazama kule walikofika, Lupita aliandika.

Makumi ya wanawake katika sekta ya uigizaji wamejitokeza kudai kwamba walinyanyaswa kijinsia na bwana Weinstein , madai ambayo amekana.

Idara ya polisi mjini Los Angeles ilitangaza katika mtandao wa Twitter siku ya Alhamisi kwamba imemfungulia uchunguzi mtayarishaji huyo wa filamu kuhusu madai ya ubakaji.

Msemaji wa polisi alimabia kituo cha habari cha AFP kwamba idara hiyo ilimuhoji muathiriwa wa unyanyasji wa kijinsia ambaye aliripoti kisa kilichotokea 2013.

Uchunguzi unaendelea na hawezi kujibu swali lolote kuhusu ni lini mahojiano hayo ama kisa hicho kilifanyika.