Kwa Picha: Afrika wiki hii 13-19 Oktoba 2017

Mkusanyiko wa picha bora kutoka Afrika na kuhusu Waafrika kote duniani wiki hii.

Sandra Kouadio poses with her hairstyle in Abidjan, Ivory Coast, October 13, 2017.

Chanzo cha picha, Reuters

Nchini Ivory Coast katika mji mkuu wa kibiashara Abidjan, Sandra Kouadio anajiweka sawa kupigwa picha akiwa na mtindo wake wa karibuni zaidi wa nywele...

Chanzo cha picha, Reuters

Naye Simon Nkendoh anasubiri wateja katika duka lake la ususi jijini humo.

Chanzo cha picha, AFP

Na siku iliyofuata nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, katika mji wa Kinshasa, wanamitindo wanajiandaa kujitokeza kwenye jukwaa wakati wa maneosho ya mitindo ya Kinshasa Fashion Week...

Chanzo cha picha, AFP

Baadhi ya waliopewa kazi ya kuwapamba wanamitindo walilazimika kutumia taa za simu wakati wa kuwapodoa na kuwarembesha...

Chanzo cha picha, JOHN WESSELS

Mwanamitindo huyu baadaye alijitokeza jukwaani, akionesha mavazi ambayo yalitengenezwa na mbunifu kutoka nchi hiyo

Chanzo cha picha, EPA

Na Jumatano, wanaume hawa wanashiriki katika maonesho mbio za farasi katika jiji la el-Jadida city, kusini mwa Casablanca...

Chanzo cha picha, EPA

Wakati wa maonesho hayo, wapanda farasi huwaongoza kukimbia sambamba na kwa kasi sawa, kisha wanaongeza kasi. Wapanda farasi kisha hufyatua risasi zao hewani wakitumia bunduki za zamani.

Chanzo cha picha, AFP

Na Alhamisi, wacheza ngoma wa kitamaduni wanajipamba kabla ya kutumbuiza katika sherehe za Diwali, sikukuu ya Wahindi, katika mji wa Durban, Afrika Kusini.

Chanzo cha picha, AFP

Na hapa, siku ya Jumanne, wachezaji dansi hawa wanatumbuiza wakati wa kufunguliwa kwa mkutano wa Wake wa Marais wa Afrika Magharibi, ambao mwaka huu uliangazia kampeni dhidi ya ajira ya watoto..

Chanzo cha picha, EPA

Na siku iliyofuata mjini Monrovia, Liberia, watoto hawa wanabeba ujumbe wa usawala wa jinsia vichwani.

Chanzo cha picha, EPA

Siku moja awali, wakazi walionekana wakifuatilia matokeo ya uchaguzi wa urais katika ubao kwenye makutano ya barabara mjini. Uchaguzi wa marudio utafanyika mwezi ujao kati ya George Weah na Joseph Boakai.

Chanzo cha picha, EPA

Na Johannesburg siku ya Jumatatu, wakazi hawa wanaonekana wakitembea kupitia eneo lenye maduka na vyumba vilivyojengwa kwa makontena katika mtaa wa Maboneng.

Chanzo cha picha, EPA

Mtaa huo kwa sasa umeanza kuinuka, kupitia mpango wa ustawishaji ambao unaendeshwa na maafisa wa jiji.

Chanzo cha picha, AFP

Na Jumamosi, nyota wa soka wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang anasherehekea baada ya kufunga bao mechi kati ya Dortmund na RB Leipzig.

Picha kwa hisani ya AFP, EPA, PA na Reuters