WHO lamteuwa Mugabe kuwa balozi mwema wa afya

Rais Robert MUgabe ateuliwa kuwa balozi mwema wa fya na shirika la afya duniani WHO Haki miliki ya picha Getty Images/AFP
Image caption Rais Robert MUgabe ateuliwa kuwa balozi mwema wa fya na shirika la afya duniani WHO

Shirika la afya duniani WHO limemteuwa rais wa Zimbabwe Robert Mugabe kama 'balozi mwema ' katika kusaidia kukabiliana na magonjwa yaliyosahaulika .

Akifafanua uamuzi wa uteuzi huo , Mkurugenzi mkuu mpya wa W.H.O., Dr Tedros Adha-nom Ghebre-yesus, alisifu namna Zimbabwe inavyozingatia afya ya umma.

Lakini wakosoaji wanasema katika kipindi cha miaka thelathini na saba ya utawala wa rais Mugabe, huduma za afya zimekuwa mbaya ambapo wahudumu wa afya wamekuwa hawalipwi mara kwa mara , na kumekuwa na ukosefu mkubwa wa dawa muhimu .

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wakosoaji wanasema kuwa sekta ya afya ya Zimbabwe imekuwa aiafikii viwango vya afya nchini humo

Dr .Tedros, ni raia wa Ethiopia ambaye ni Muafrika wa kwanza kuongoza shirika la W.H.O. na alichaguliwa kwa ajili ya kukabiliana na kile kilichoaminiwa kuwa ni kugeuzwa kwa shirika hilo kuwa la kisiasa.

Mada zinazohusiana