Maafisa 53 wa usalama wauawa na wapiganaji Misri

Shambulio hilo lilitokea katika eneo la jangwa Haki miliki ya picha AFP
Image caption Shambulio hilo lilitokea katika eneo la jangwa

Maafisa nchini Misri wanasema kuwa takiban maafisa 53 wa usalama na wapiganaji wa kiislam kumi na watano wameuawa katika makabiliano yaliyotokea katika eneo la jangwa magharibi mwa nchi hiyo .

Wizara ya mambo ya ndani nchini humo inasema kuwa wapiganaji waliwafyatulia risasi wanajeshi wakati walipokuwa wakifanya uvamizi kwenye maficho yao, karibu na eneo lenye chemi chemi Bahariya .

Duru za usalama zinasema kuwa wapiganaji walikuwa na uelewa zaidi wa eneo hilo na afisa wa kijeshi aliyetoa maagizo ya uvamizi alishindwa kuagiza wanajeshi kuimarisha kikosi chake .

Taarifa moja inasema kuwa wapiganaji hao ni wajumbe wa kikundi kinachofahamika kama Hasm, ambacho kiliwahi kuyashambulia majeshi ya usalama awali.

Mada zinazohusiana