Chelsea yatoka nyuma na kuilaza Watford

Beki wa Chelsea Azpilicuetta baada ya kufunga bao lake dhidi ya Watford Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Beki wa Chelsea Azpilicuetta baada ya kufunga bao lake dhidi ya Watford

Mkufunzi wa Chelsea Antonio Conte amesema timu yake ilionyesha ujasiri wa kupigania ushindi baada ya kufunga mabao mawili dakika za lala salama na kutoka nyuma na kupata ushindi dhidi ya Watford katika uwanja wa Stamford Bridge.

Cesa Azpilicueta aliifungia Chelsea bao la tatu katika dakika ya 87 kabla ya Mitchy Batshuayi kufunga udhia katika dakika ya mwisho hivyobasi kumaliza msururu wa mechi tatu bila ushindi licha ya kutocheza vizuri.

Lilikuwa bao la pili la Batshuayi baada ya kufunga bao la kusawazisha kupitia kichwa kizuri katika kipindi cha pili licha ya timu yake kufungwa bao kila kipindi cha mchezo.

Pedro aliifungia timu hiyo ya nyumbani bao la kwanza katika dakika ya 12 baada kupiga mkwaju mkali akiwa maguu 25 ambao ulimwacha bila jibu kipa Heurelho Gomes .

Lakini safu ya ulinzi ya Blues ilikuwa ikiteteleka mara hivyobasi Watford ilifunga mara mbili kupitia Abdoulaye Doucoure na Robert Pereyra ili kuwaweka kifua mbele.

Mada zinazohusiana