Marais 5 wa zamani wakutana kuchangisha fedha Marekani

Five former U.S. presidents, Jimmy Carter, George H.W. Bush, George W. Bush, Bill Clinton, and Barack Obama attend a concert at Texas AM University benefiting hurricane relief efforts in College Station, Texas, U.S., 21 Octobe, 2017 Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Marais wa zamani Jimmy Carter, George H.W. Bush, George W. Bush, Bill Clinton, na Barack Obama

Marais watano wa zamani nchini Marekani wamekusanyika kwenye warsha ya kuwasaidia waathiriwa wa janga la kimbunga ambacho kilikumba maeneo kadha ya Marekani.

Barack Obama, George W Bush, Bill Clinton, George HW Bush na Jimmy Carter wote walikutana Texas siku ya Jumamosi.

Wedemocrat watatu wa Warepulican wawili walikutana warsha ya Amerika moja yeye lengo la kuwasaidia wale walikumbwa na janga la vimbunga Irma na Maria.

Warsha hiyo imechangisha dola milion 31 hadi sasa.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Lady Gaga akiimba katika tamasha

Wanasiasa hao walizindua mchango huoa baada ya kibunga Harvey ambacho kilisababisha uharibifu wa mabilioni ya fedha kilitua katika jimbo la Texas Agosti.

Mchango huo sasa utasaidia jamii za Florida, Puerto Rico na viswa vya Marekani vya Virgin vilivyopigwa na kibunga.

Hata hivyo Rais Trump hakuhudhuria, lakini alituma ujumbe kabla na kuwapongeza marais hao kwa kazi yao nzuri.

Obama na Bush awali wametoa hotuba na kuukashifu utawala wa Trump.

Mada zinazohusiana