Rais wa Catalonia anasema hatakubali mipango ya Uhispania

Puigdemont Haki miliki ya picha AFP/Getty
Image caption Bw Puigdemont alisema Madrid imekataa mazungumzo

Rais wa Catalonia Carles Puigdemont, anasema eneo hilo haliwezi kukubali mipango wa Madrid ya utawala wa moja kwa moja.

Alisema kuwa hilo ni shambulizi kali dhidi ya idara za Catalonia tangu utawala wa kiimla wa Jenerali Franco wa mwaka 1939-1975, ambapo uongozi wa eneo hilo ulifutwa.

Uhispania yatoa vitisho kwa Catalonia

Mipango ya waziri mkuu Mariano Rajoy ni pamoja na kuwaondoa viongozi wa Catalonia na kulivunja bunge.

Alisema ataitisha bunge la Catalonia kujadili jibu kwa mipango ya Bwa Rajoy.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Bw Rajoy alisema serikali itatumia kipengee cha 155 cha katiba

Polisi wa Barcelona walisema kuwa watu 450,000 waliandamana kwenye mji mkuu mapema Jumamosi wengi wakiimba"Uhuru".

Ripoti zinasema kuwa wizara ya masuala ya ndani inajiandaa kuchukua udhibiti wa polisis wa Catalonia na kumuondoa kamanda wake Josep Lluís Trapero, ambaye tayari anakabiliwa na mashtaka ya uhaini.

Serikali pia itatathmini kuchukua udhibiti wa kituo cha televisheni cha TV3 na gazeti la El País.

Mada zinazohusiana