Mamilioni wapiga kura Japan huku tisho la kimbunga likiongezeka

A girl stands next to her father filling out his ballot for a national election at a polling station in Tokyo, Japan October 22, 2017 Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mvua kubwa imekuwa ikinyesha kusini mwa Japan hukun watu wakipiga kura

Mamilioni ya raia wa Japan, wamejitokeza kupiga kura, katika uchaguzi wa mapema, huku waziri mkuu, Shinzo Abe, akitarajiwa kushinda, licha ya kura ya maoni kuonyesha kwamba, umaarufu wake umepungua miongoni mwa wapiga kura.

Uchaguzi huo mkuu wa mapema uliitishwa na Bwana Abe, mwaka mmoja kabla ya muda rasmi wa uchaguzi mkuu kufika.

Kura hiyo ya mapema, iliyopingwa na gavana mwenye ushawishi mkubwa wa Jiji kuu- Tokyo Yuriko Koike, inaonekana kufifia.

Iwapo atashinda katika uchaguzi huo mkuu, Bwana Abe, amependekeza kufanyia marekebisho katiba ya nchi hiyo iliyobuniwa baada ya vita vikuu vya pili vya duniani inayojumuisha kuondolewa kwa kifungu cha sheria, kinachopinga Japan kuingia vitani, hasa wakati huu ambapo taifa hilo linapokea vitisho vya mara kwa mara kutoka Korea Kaskazini, ambayo mara kwa mara inafanyia majaribio zana zake za nyuklia.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Uchaguzi huo mkuu wa mapema uliitishwa na Bwana Abe, mwaka mmoja kabla ya muda rasmi wa uchaguzi mkuu kufika.

Wakati huo huo, kimbunga kikali kinaelekea kugonga taifa la Japan, huku wakaazi wanaoishi katika maeneo ya pwani wakitahadharishwa kuondoka maeneo ya nyanda za chini na kuelekea milimani na mahali salama.

Kimbunga hicho kiitwacho Lan, kinaelekea hadi kwenye visiwa vya Japan, na kinatarajiwa kugonga mji mkuu Tokyo, kesho Jumatatu.

Mamia ya safari za ndege na huduma za treni zimesitishwa, kutokana na hofu ya upepo huo mkali na mvua kubwa inayotarajiwa kunyesha.

Kampuni kubwa ya uundani magari ya Toyota, imetangaza kufunga viwanda vyake vyote nchini Japan kutokana na hatari ya kimbunga hicho.

Mada zinazohusiana