Shinzo Abe aelekea kupata ushindi mkubwa uchaguzi Japan

A girl stands next to her father filling out his ballot for a national election at a polling station in Tokyo, Japan October 22, 2017 Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mvua kubwa imekuwa ikinyesha kusini mwa Japan

Hesabu za awali katika uchaguzi mkuu wa Japan, zinaonyesha kuwa waziri mkuu Shinzo Abe, ameshinda kwa kishindo.

Takwimu zinatabiri kuwa serikali ya mseto inayoongozwa na chama cha LDP cha Bwana Abe, itapata kama thuluthi mbili za viti vya bunge.

Bwana Abe aliitisha uchaguzi, ili kupata idhini ya raia wakati tishio kutoka Korea Kaskazini linazidi.

Pia ameahidi kuacha sera ya Japan ya kutojihusisha na vita, na kuzidisha mchango wa jeshi.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Uchaguzi huo wa mapema uliitishwa mwaka mmoja kabla

Ushindi huo, utamaanisha kuwa Bwana Abe atakuwa waziri mkuu aliyetumika muda mrefu kabisa Japan.

Waliojitokeza kupiga kura hawakuwa wengi, kwa sababu ya kimbunga.

Mamia ya safari za ndege na huduma za treni zimesitishwa, kutokana na hofu ya upepo huo mkali na mvua kubwa inayotarajiwa kunyesha.

Kampuni kubwa ya uundani magari ya Toyota, imetangaza kufunga viwanda vyake vyote nchini Japan kutokana na hatari ya kimbunga hicho.

Mada zinazohusiana