Jitihada za kutokomeza ndoa za utotoni Afrika Magharibi na Kati

Ndoa za utotoni Haki miliki ya picha Getty Images

Senegal ni mwenyeji wa mkutano wa siku tatu utakaonza hii leo wenye lengo la kuongeza hatua za kutokomeza ndoa za utoto katika nchi za Afrika Magharibi na Kati.

Mashirikia ya misaada yanasema, katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na hatua zinazoleta matumaini, lakini eneo hilo bado lina nchi kati ya sita mpaka kumi ambazo zina kiwango kikubwa cha ndoa za utotoni duniani kote.

Ndoa za utoto badi ni jambo la kawaida katika nchi za Afrika Magharibi na Kati huku takwimu zikionyesha asimilia 76 ya watoto wa kike chini ya umri wa miaka 18 wakiolewa kwa nguvu nchini Niger, asilimia 68 katika Jamhuri ya Afrika ya Kati na Chad, na zaidi ya asilimia 50 nchini Mali na Guinea.

Mara nyingi mabinti wanaoolewa huwa wameacha shule, na kupata elimu kwa watoto hao inaaminika kuwa ndio njia pekee ya kupambana na tatizo la ndoa za utotoni.

Wazazi ambao hali zao ni duni, mara nyingi huwaozesha watoto wao mapema ili kupunguza mzigo wa ulezi, wakati huo huo, baadhi ya imani za dini zinathamini watoto kuolewa mapema.

Mkutano huu, unajumuisha mawaziri wa serikali mbalimbali, viongozi wa dini na wa mila pamoja na mashirika ya Umoja wa Mataifa na yal yanayotoa msaad huku lengo likiwa ni kutafuta mbinu zitakazo maliza tatizo hilo.