Mwili wa mtoto wa miaka 3 aliyefukuzwa nyumbani usiku wapatikana Texas

Police searching for Sherin Mathews Haki miliki ya picha Richardson police department/Facebook
Image caption Maafisa waliokuwa wakimtafuta mtoto Sherin

Polisi huko Texas wanasema kuwa wamepata mwili wa mtoto wa miaka mitatu Sherin Mathews ambaye alitoweka tarehe 7 mwezi huu, wakati babake alimfukuza kutoka nyumbani kwao mwenda saa tatu usiku kama njia ya kumuadhibu.

Polisi waliwaambia waandishi wa habari kuwa mwili huo ulionekana kuwa wa Sherin ambaye habari za kutoweka kwake zilisambaa mjini Dallas na India.

Wanandoa hao kutoka India walimpangisha mtoto huyo miaka miwli iliyopita kutoka makao ya kuwatunza watoto nchini India.

Polisi hata hivyo hawajatoa taarifa kuhusu ni kipi kilisababisha mtoto huyo arafariki.

Mwili huo ulipatikana kwenye andaki kuribu nusu maili kutokan nyumbani kwao siku ya Jumamosi.

Babake Sherif, Wesley Mathews alikamatwa na kuachiliwa kwa dhamana, kwa kuhatarisha maisha ya mtoto huyo baada ya kumfukuza kutoka nyumbani usiku kutokana na sababu kuwa alikataa kumaliza maziwa aliyokuwa akinywa.

Mamake anasemakana kuwa alikua akilala wakati kisa hicho kilitokea.

Wanandoa hao wana mtoto mwingine wa miaka minne ambaye alichukuliwa kutunzwa baada ya kisa hicho.

Mada zinazohusiana