Mpiga mbizi aogelea kilomita 7.5 baada ya kuachwa na mashua Australia

John Craig embraces his wife after surviving a 7.5km swim back to shore Haki miliki ya picha GLEN RIDGLEY
Image caption John Craig akimkumbatia mkewe baada ya safari ndefu ya kuogelea

Mpiga mbizi mmoja raia wa Uingereza alilazimika kuogelea umbali wa kilomita 7.5 kwenda ufukweni nchini Australia baada ya kupoteleana na mashua yake huku akifuatwa na papa.

John Craig, 34, amelikuwa akivua samaki kwa kutumia mkuki magharibi mwa Autralia siku ya Ijumaa, lakini wakati alipoibuka kutoka kwenye maji hakuiona tena mashua ambayo ilikuwa ikiendeshwa na rafiki yake.

Bw. Craig alisema alimuona nyangumi alipokuwa akiomba msamaha.

Haki miliki ya picha John Craig
Image caption John Craig

Kisha akaanza safari ndefu ya kuogelea kwenda ufukweni kabla ya kufika ardhini na kutembe kwa karibu kilomita 30 hadi alipoonekana.

Mwanamume huyo mwenye ujuzi wa kupiga mbizi alihamia Australia miaka miwili iliyopita.

"Papa huyo alishinda akinikaribia kutoka pande zote. Alikuwa anajaribu kufahamu mimi ni nani au labda ningekuwa chakula chake." aliiambia BBC.

"Niliogopa. nilifikiri ningeliwa baharini, nyangumi huyo alishinda akinifuata."

Image caption Magharibi mwa Australia

Mada zinazohusiana