Maisha ya pacha waliozaliwa wameshikana hatarini Gaza

Palestinian conjoined twins lie in an incubator at the nursery of the Shifa Hospital in Gaza City (02 October 2017) Haki miliki ya picha AFP
Image caption Watoto hao walizaliwa Jumamosi na mmoja wao anatajwa kuwa dhaifu kuliko mwingine.

Maisha ya watoto pacha waliozaliwa wakiwa wameshikana yako hatarini iwapo hawataondolewa ukanda wa Gaza, kwa mujibu wa madaktari.

Alam Abu Hamna kutoka hspitali ya Shifa, ilisema kuwa hali inayowakumba watoto hao wasichana ni ngumu na kwamba haiwezi kutatuliwa na madaktari wa hospitali zilizo ukanda wa Gaza.

Ilisema kuwa matumaini ni kuwa watoto hao watasafirishwa ng'ambo ili watenganishwe

Watoto hao walizaliwa Jumamosi na mmoja wao anatajwa kuwa dhaifu kuliko mwingine.

Hata hivyo kila mmoja ana moyo wake na mapavu. Mapacha ambao hutumia kiungo kimoja mara nyingi hukumbwa wna hatari ya kuishi.

"Maisha yao yako hatarini, ni hali iliyo ngumu," Dr Abu Hamna alinukuliwa akisema na gazeti la Times la Israel.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Watoto hao walizaliwa Jumamosi na mmoja wao anatajwa kuwa dhaifu kuliko mwingine.

Alisema hali ya mmoja wa mapacha hao iko shwari la mwenzake yuko hali mbaya na anahitaji matibabu.

"Ikiwa watasafirishwa nje kwa haraka kupata matibabu nje, maisha yao yataokolewa," alisema.

Kitengo cha jeshi la Israel kinachohusika na kuratibu kuingia na kuondoka ukanda wa Gaza kinasema kuwa hakijapokea ombi lolote la mapacha kuondolewa eneo hilo.

Mapacha waliozaliwa wakiwa wameshikana katika Ukanda wa Gaza mwezi Novemba mwaka 2016 baadaye walikufa.

Israeli na Misri wameka vizuizi vya ardhini na baharinin kwa Ukanda wa Gaza kwa miaka kumi katika jitihada za kuzuia mashambulizi kutoka kwa wanamgambo.