Matukio muhimu baada ya uchaguzi wa urais kufutwa Kenya

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mamilioni ya wakenya walipiga kura

Wakenya wanaelekea katika vituo vya kupiga kura siku ya Alhamisi kwa marudio ya uchaguzi wa urais ambao ulifutwa na mahakama ya juu, kutokana na sababu kuwa uchaguzi huo haukuendeshwa kwa njia iliyostahili. Haya ni mambo muhimu kwenye uchaguzi huo.

Misukosuko siku ya uchaguzi

Wapiga kura walijitokeza kwa wingi tarehe 8 Agosti baada kinyangayro kikali kati ya Rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga mshindani wake wa muda mrefu.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais Kenyatta akipiga kura

Kulikuwa na hofu kuwa kampeni hizo kali zingeweza kusababisha ghasia. Zaidi ya watu 1,100 waliuawa wakati wa ghasia zilizochochewa kisiasa mwaka 2007.

Matokeo ya mapema yalimpa Kenyatta uongozi lakini yakakataliwa mara moja na Raila Odinga ambaye alidai kuwa wadukuzi waliingia katika mitambo ya teknolojia ya tume ya uchaguzi na kubadilisha matokeo.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Bw Odinga akipiga kura

Matokeo rasmi yaliyochapishwa tarehe 11 mwezi Agosti yalimpa Kenyatta asilimia 54.27 huku Odinga akipata asilimia 44.74

Ghasia hizo zilidumu muda wa siku nne na makundi ya kupigania haki za binadamu yanasema watu 37 waliuawa wengi na polisi.

Kufutwa matokeo wa kihistoria

Odinga akapeleka malalamiko yake katika mahakama ya juu. Kwenye uamuzi wa kushangaza tarehe 1 mwezi Septemba, majaji walifuta matokeo hayo na kuamrisha marudio ya uchaguzi ndani ya siku 60.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Jaji mkuu Kenya David Maraga

Tarehe ya uchaguzi ilitangazwa kuwa 17 Oktoba. Barua ya siri ambapo tume ya IEBC ilikiri kuwepo matatizo na kushindwa kuandaa uchaguzi kwa njia inayofaa ilitokea kwa umma tarehe 7 mwezi Septemba.

Uchaguzi ukaahirishwa

Baada ya mahaka kuu kutoa hukumu kamili na kuilaumu tume ya uchaguzi kwa kuendesha uchaguzi kwa njia isiyofaa, IEBC ilitangaza kusongesha mbele tarehe ya marudio ya uchaguzi hadi tarehe 26 Oktoba ili kujiaindaa.

Mkuu wa mashtaka nchini Kenya tarehe 23 Septemba akaamrisha uchunguzi kwa tume ya IEBC.

Odinga ajiondoa kwenye uchaguzi

Maandamano yalizuka mapema Oktoba wakati Bw. Odinga alitoa wito kwa wafuasi wake kuishinikiza serikali kuifanyia tume ya uchaguzi mabadiliko. Takriban watu watatu waliuawa kwenye ghasia ambazo zilifuata.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mwenyekiti wa IEBC

Tarehe 10 Oktoba Odinga alijiondoa kwenye kinyanganyiro hicho akisema kuwa IEBC imeshindwa kufanya mabadiliko yanayohitajika.

Lakini pia akasema kuwa vita vyake havikushia hapo, akisema ipo sheria ambayo chama chake kinaamini inaweza kuishinikiza IEBC kuandaa uchaguzi mpya kutoka mwanzo.

Kamishina ajiuzulu

Mmoja wa makamishina saba wa tume ya uchaguzi Roselyn Akombe alitangaza kujiuzulu tarehe 18 mwezi Oktoba ambapo pia aliikimbia nchi.

Naye mwenyekiti wa tume ya IBEC akaelezea shaka kwa tume hiyo kuandaa uchaguzi ulio wa haki na kulaumu pande zote kwa kuingilia tume.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kamishina aliyejiuzulu Roselyn Akombe

Odinga aliuambia umati kwenye mkutano mkubwa siku hiyo hiyo kuwa hakutakuwa na uchaguzi na kuitisha maandamano ya nchi nzima siku ya uchaguzi.

Lakini siku iliyofuatia alisema atafikiria upya uamuzi wake wa kususia uchaguzi na kutangaza uamuzi siku moja kabla ya uchaguzi.